RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya katika Mikoa ya Tanzania Bara. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Uteuzi huo, umetangazwa leo Jumamosi, tarehe 19 Juni 2021 kupitia taarifa kwa umma, iliyotolewa na Jaffar Haniu, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu.
Miongoni mwa walioteuliwa ni waliokuwa wabunge na wanachama wa upinzani, ambao waliunga juhudi na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na waandishi wa habari.
Baadhi ya waliokuwa wabunge wa upinzani ambao wameteuliwa kuwa wakuu wa wilaya ni Peter Lijualikali, Joshua Nassari na Dk. Vicent Mashinji ambaye yeye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Chadema.
Waandishi wa habari ni; Fatma Nyangasa pamoja na Simon Simalenga.
Orodha yote ya wakuu wa wilayani hii hapa;
Leave a comment