RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya (DC) wawili. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Uteuzi huo, umetangazwa jana Jumanne, tarehe 22 Juni 2021 na Jaffar Haniu, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.
Walioteuliwa ni; Suleiman Yusuph Mwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida.
Mwenda anachukua nafasi ya Kenan Kihongosi ambaye kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imemteua kuwa Katibu Mkuu wa umoja wa vijana wa chama hicho (UVCCM).
Kabla ya uteuzi huo, Mwenda alikuwa Katibu Msaidizi Idara ya Oganaizesheni ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Makao Makuu jijini Dodoma.
Aidha, Rais Samia amemteua, Lupakisyo Andrea Kapange kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu.
Kapange anachukua nafasi ya Dk. Charles Mhina ambaye atapangiwa majukumu mengine.
Kabla ya uteuzi huo, Kapange alikuwa Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Tanga.
Leave a comment