Wednesday , 29 March 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Rais Samia ateua Katibu Mtendaji NECTA
Elimu

Rais Samia ateua Katibu Mtendaji NECTA

Spread the love

 

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Dk. Said Ally Mohamed kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo tarehe 25 Februari 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus.

Kwa mujibu wa taarifa ya Yunus, uteuzi wa Dk. Mohamed aliyekuwa Mkurugenzi wa Huduma za Ufundishaji, Mafunzo na Mitihani katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), umeanza tarehe 23 Februari mwaka huu.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Dk. Mohamed kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania. Uteuzi huu umeanza tarehe 23 Februari 2023,” imesema taarifa ya Yunus.

Dk. Mohamed anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Charles Msonde ambaye Mei 2022 aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI (elimu).

Nafasi hiyo ilikuwa ikikaimiwa na Athuman Amasi tangu kuondoka kwa Dk. Msonde.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari

Serikali yataka vijana  wajiunge na program atamizi ya biashara CBE

Spread the love  SERIKALI imewahamasisha vijana kujiunga na program atamizi inayotolewa na...

Elimu

Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini wamwaga mamilioni ujenzi maabara za sekondari

Spread the love  MFUKO wa Jimbo la Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara,...

ElimuHabari

CBE yaanzisha Shahada 10 za Uzamili, CBE yajivunia wahitimu wanaoajirika

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimewataka wenye  kampuni na...

Elimu

Harambee ujenzi sekondari za Musoma Vijijini yashika kasi

Spread the love  HARAMBEE ya ujenzi na ukarabati wa shule za sekondari...

error: Content is protected !!