May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia ateua ‘Boss’ mpya FCC, WCF

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewateua watendaji wakuu katika Tume ya Ushindani wa Biashara (FCC) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Uteuzi huo umetangazwa jana tarehe 29 Mei 2021 na Mkurugenzi wa Mwasiliano ya Rais-Ikulu, Gerson Msigwa.

Taarifa ya Msigwa imesema, Rais Samia memteua  William Erio, kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa FCC.

Kabla ya uteuzi huo,  Erio alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Pia, Rais Samia amemteua alikuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa FCC,  Dk. John Kedi Mduma, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa WCF.

error: Content is protected !!