Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali na kutengua uteuzi wa Dk. Fenella Mukangara, aliyewahi kuwa waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Uteuzi huo, umetangazwa leo Alhamisi, tarehe 23 Desemba 2021 na Jaffar Haniu, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.
Miongoni mwa walioteuliwa ni Profesa Othuman Chande Othuman kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Profesa Othuman ni mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anachukua nafasi ya Dk. Fenella ambaye uteuzi wake umetenguliwaz
Taarifa yote ya uteuzi hii hapa;
Leave a comment