November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia ateua 8, yumo bosi wa zamani SSRA

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi nane akiwemo bosi wa zamani wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Dk. Irene Isaka. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Isaka ameteuliwa kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA).

Dk. Isaka alitenguliwa SSRA akiwa mkurugenzi mkuu Desemba 2018 na aliyekuwa Rais wa wakati huo, Hayati John Pombe Magufuli.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Ni baada ya kuibuka kwa mjadala mkali kuhusu kikokotoo cha mafao ya wastaafu.

Uteuzi wa Dk. Isaka na wenzake, umetangazwa leo Jumamosi tarehe 13 Novemba 2021 na Jaffar Haniu, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu.

Taarifa ya walioteuliwa wote hii hapa:-

error: Content is protected !!