Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia ateta na mjumbe wa UN
Habari za Siasa

Rais Samia ateta na mjumbe wa UN

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya mazungumzo na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Dk. Phumzile Mlambo-Ngouka, kuhusu mikakati mbalimbali ya kuwainua wanawake nchini. Anaripoti Nasra Bakari, DMC … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Gerson Msigwa, mazungumzo hayo yamefanyika leo Ijumaa, tarehe 28 Mei 2021, katika Ikulu ya jijini Dar esSalaam.

“Leo Rais Samia amekutana na kufanya mazungumzo na Msaidizi wa Katibu Mkuu UN, Dk. Ngouka, kuhusu kuendeleza agenda zinazowahusu wanawake,” imesema taarifa ya Msigwa.

Katika mazungumzo hayo, Dk. Phumzile alimualika Rais Samia ashiriki katika mkutano utakaojadili masuala ya kijinsia, uliopangwa kufanyika tarehe 30 Juni 2021 huko Paris nchini Ufaransa.

“Mkutano huo madhumuni yake ni kuchagiza usawa wa kijinsia kama yalivyokubaliwa katika mkutano wa Beijing uliofanyikamwaka 1995 baada ya kuonekana baadhi ya maazimio yanasuasua,” imesema taarifa ya Msigwa.

Kwa upande wake Rais Samia, alikubali ombi la Dk. Phumzile la kushiriki mkutano huo, sambamba na kuwa kiongozi katika mjadala wa haki za kiuchumi.

“Kuelekea mkutano huo nchi zitakazoshiriki zimegawanywa katika maeneo sita ya kufanyia kazi na Rais Samia amekubali kuwa kiongozi katika eneo la haki za kiuchumi,” imesema taarifa ya Msigwa.

Pia, Rais Samia amelipongeza Shirika la Umoja wa Mataifalinaloshughulikia masuala ya Wanawake (UN-Women), kwa juhudi zake za kupigania masuala ya wanawake, ikiwemo maazimio ya Beijing.

“Rais Samia ameeleza kuwa, Tanzania ipo tayari kuungana na UN-Women katika kuongeza msukumo wa utekelezaji wake. Amebainisha kuwa japo Tanzania bado haijafikia kiwango cha usawa wa kijinsia cha 50/50 katika uongozi, katika kipindi chake atahakikisha anaongeza jitihada za kufikia usawa huo,” imesema taarifa ya Msigwa na kuongeza:

“Rais Samia ameishukuru UN-Women, kwa utayari wake wa kuisaidia Tanzania katika kukabiliana na janga la ugonjwa wa Korona (Covid-19).”

1 Comment

  • Hongera kwa kuvaa barakoa SSH. Sasa toa agizo kwa Watanzania nao wafuate maagizo ya wataalamu. Tubadilike Covid 19 IPO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

error: Content is protected !!