Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia ateta na kigogo AU
Habari za Siasa

Rais Samia ateta na kigogo AU

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo Jumamosi, tarehe 11 Desemba 2021, amefanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC), Moussa Faki Mahamat, Ikulu jijini Dar es Salaam. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa juu ya mazungumzo hayo, imetolewa mchana wa leo kwa umma na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Jaffar Haniu.

Taarifa ya Haniu imesema kuwa, Rais Samia amemueleza Faki kwamba, Tanzania inajitahidi kukabiliana na athari za kiuchumi, zilizotokana na Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19), ili kuhakikisha uchumi wake unaimarika.

“Rais Samia amesema ni wakati sasa kwa nchi za Afrika, kiutumia fursa zilizopo baada ya athari za UVIKO-19, kujiimarisha kiuchumi, kwa sababu nchi zina fursa nyingi kiuchumi,” imesema taarifa ya Haniu.

Katika mazungumzo hayo, mwenyekiti huyo wa Kamisheni ya AU, ameishauri Tanzania kuchangamkia fursa zinazopatikana katika Eneo Huru la Biashaea Afrika (AfCFTA)

“Faki amesema anategemea kama Tanzania ilivyokuwa kinara kweye ukombozi wa Afrika, basi itakuwa kinara pia katika kuchangamkia fursa ya AfCFTA , katika kukuza biashara ikizingatiwa kuwa, kupitia miundombinu yake ya bandari imeweza kuimarisha biashara na nchi jirani,” imesema taarifa ya Haniu.

Faki amesema kuwa, Tanzania ni kitovu muhimu cha kuunganisha nchi jirani kibiashara na uysafirishaji biadhaa mbalimbali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!