Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Rais Samia ateta na bosi AfDB, wakubaliana haya
Habari Mchanganyiko

Rais Samia ateta na bosi AfDB, wakubaliana haya

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dk. Adesina Akinumwi amemhakikishia, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kuwa benki hiyo itaendelea kufadhili miradi ya maendeleo. Anaripoti Nasra Bakari, DMC … (endelea).

AfDB imesema, ipo tayari kufadhili miradi mipya kwa kuwa Tanzania ina sifa za kuendelea kupata ufadhili.

Dk. Adesina aliyepo jijini Abidjan nchini Ivory Coast, amesema hayo leo Ijumaa, tarehe 11 Juni 2021, wakati akizungumza kwa njia simu na Rais Samia aliyepo jijini Dar es Salaam kuhusu uhusiano wa Tanzania na benki hiyo ambayo imekuwa ikifadhili miradi mbalimbali ya maendeleo.

Katika mazungumzo hayo, Dk. Adesina ambaye ameanza kwa kutoa pole kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Magufuli na kutoa pongezi kwa Rais Samia kwa kupokea kijiti cha Urais amesema, Tanzania inafanya vizuri katika uchumi na ana matumaini makubwa Rais Samia ataendeleza jitihada zilizokuwa zikifanywa na mtangulizi wake.

Ameahidi AfDB itatoa ufadhili kwa Tanzania ili kuanzisha benki za wajasiriamali zitakazowakopesha vijana wanaohitimu mafunzo ya ufundi stadi pamoja na kujihusisha na kilimo, jambo litakalosaidia kupungua kwa tatizo la ajira kwa vijana na kuwaongezea kipato.

Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dk. Adesina Akinumwi

Aidha, Dk. Adesina amemualika Rais Samia kuhudhuria mkutano wa uwekezaji utakaowaleta wawekezaji wakubwa pamoja ambao unatarajiwa kuvutia mabilioni ya fedha kwa ajili ya kuwekeza katika nchi mbalimbali.

Pia, Dk. Adesina amesema, AfDB imetenga dola za Marekani bilioni tano kwa ajili ya kusaidia wanawake na ameomba Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa uwezeshaji wanawake kiuchumi ambapo Rais Samia amekubali ombi hilo.

Dk. Adesina ameahidi kuleta wataalamu wa benki hiyo hapa nchini ili wakutane na wataalamu wa Tanzania kwa ajili ya kupitia miradi ambayo tayari inafadhiliwa na benki hiyo na kujadili fursa za kuanzisha miradi mipya.

Kwa upande wake, Rais Samia amemshukuru Dk. Adesina kwa salamu zake za pole na pongezi na amemshukuru kwa benki hiyo kufadhili miradi mingi ya maendeleo hapa nchini ikiwemo inayotekelezwa chini ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa awamu ya pili na amemhakikishia kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na benki hiyo.

Ameelezea kufurahishwa kwake na mradi wa AfDB wa kufadhili vijana wanaojihusisha na kilimo na wanaomaliza mafunzo katika vyuo vya ufundi stadi kwa kuwa ufadhili huo utawawezesha vijana wengi wa Tanzania kuzalisha mali.

Pamoja na kumpongeza Dk. Adesina kwa ushindi wake wa kuchaguliwa kuwa Rais wa AfDB kwa kipindi cha pili, Rais Samia amemuomba kuongeza nafasi za Watanzania wanaoajiriwa katika benki hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanafunzi Nyamkumbu wanolewa na GGML kuhusu taaluma ya madini

Spread the loveZAIDI ya Wanafunzi 50 kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana...

Habari Mchanganyiko

Somo la dini: Waislamu waishukia Serikali, wizara yatoa kauli

Spread the loveJUMUIYA na Taasisi za Kiislamu Tanzania, imetupia lawama Serikali ikidai...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

error: Content is protected !!