May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia ateta na Angela Merkel, aahidi kutoa chanjo ya corona

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya mazungumzo kwa simu na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa ya Jaffar Haniu,Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu imesema, mazungumzo hayo yamefanyika leo Jumatano tarehe 1 Septemba 2021, akiwa Ikulu ya Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, Merkel amempongeza Rais Samia kwa kushika hatamu za Urais nchini Tanzania na kumpa pole kufuatia kifo cha Aliyekuwa Rais wa Taifa hilo, Hayati John Pombe Magufuli.

Merkel amempongeza Rais Samia kwa jitihada zake za kupambana na UVIKO- 19 na kuahidi kuunga mkono jitahada hizo kwa kutoa msaada wa chanjo za kukabiliana na ugonjwa huo.

Aidha, Merkel amesema Oktoba 2021,Serikali yake itaanzisha majadiliano na Serikali ya Tanzania kuhusu maeneo ambayo Serikali ya Shirikisho la Ujerumani inaweza kusaidia kutokana na athari za UVIKO 19.

Pia, Merkel amempongeza Rais Samia kwa jitihada zake za kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini ambapo ameahidi kuwashawishi wafanyabiashara wa Ujerumani na watalii kutembelea na kuwekeza nchini Tanzania.

Kwa upande wake, Rais Samia amemshukuru Merkel kwa ushirikiano wake na Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo.

Rais Samia amempongeza Merkel kwa kumaliza kipindi chake cha uongozi akiwa ni kiongozi wa kisiasa mwanamke aliyeongoza muda mrefu ndani ya Chama chake cha CDU na ndani ya Jumuiya ya Ulaya.

error: Content is protected !!