Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Samia atengua wawili, Mchechu wa NHC awa Msajili wa Hazina
Habari Mchanganyiko

Rais Samia atengua wawili, Mchechu wa NHC awa Msajili wa Hazina

Nehemiah Mchechu, Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
Spread the love

 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi wa Msajili wa Hazina, Mgonya Benedicto na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk. James Mataragio. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa tarehe 24 Februari 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus, imeeleza kuwa wawili hao watapangiwa nafasi zingine.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Samia amemteua aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Mchechu kuwa Msajili wa Hazina akichukua nafasi ya Benedicto.

Pia Rais Samia amemteua Mussa Mohammed Makame, kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC akichukua nafasi ya Dk Mataragio. Kabla ya uteuzi huo, Makame alikuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), na pia ni Mshauri Mwelekezi wa masuala ya mafuta na gesi nchini Tanzania.

Aidha Rais Samia amemteua Hamad Abdallah, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) akichukua nafasi ya Mchechu ambaye ameteuliwa kuwa Msajili wa Hazina. Kabla ya uteuzi huo, Abdallah alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Gimcoafrica Limited.

1 Comment

  • Rais Samia bila shaka alijua kuwa Mchechu alitenguliwa kutoka NHC na JPM hata hivyo akamrejesha. Bila shaka angeangalia mafaili ya siri angegundua sababu ya Mchechu kuenguliuwa. Iweje tena amrejeshe NHC??? Lazima JPM alikuwa na sababu a Samia alijua hayo lakini Samia alidharau. Sasa anamuengua kutoka NHC

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!