May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia ataka wanawake kuchangamkia fursa vyuo vya ufundi

Spread the love

 

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wanawake kujifunza mafunzo ya ufundi wa ushonaji wa nguo kwa kuwa ni mojawapo ya sekta ambayo inaajiri wanawake wengi zaidi ikilinganishwa na wanaume. Anaripoti Mwandishi Wetu .. (endelea).

Pia amevitaka vyuo vya mafunzo stadi na vinavyotoa mafunzo ya fushonaji vifundishe viongozi jitihada ili kuzalisha watu wenye sifa ya kuajiriwa.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leotarehe 11 Januari, 2022 – Chumbuni Visiwani Zanzibar wakati akizindua kiwanda cha nguo cha Basra Textile Mills, ikiwa ni sehemu ya maonyesho ya kuelekea miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema uzoefu unaonyesha nchi nyingi za Bara la Asia watenda kazi wengi wanaoajiriwa kwenye viwanda vya nguo ni wanawake.

“Hii ni kwasababu wanawake ni watulivu na waangalifu sana. Kwasababu unaposhona nguo ya kimataifa haitaki papara, inataka utulie ufikie vigezo vinavyohitajika na pia mikono yao ni laini kuweka vifungo, kutunga sindano na vitu vingine.

“Lakini fikirieni mikono ya mwanaume ishike vifungo! Kwahiyo hapa ni fursa ya ajira kwa wanawake wengi. Kinamama kasomeni mshone fursa iko hapa,” amesema Rais Samia.

Aidha, amesema matarajio ni kwamba siku za usoni kuacha kuagiza bidhaa hizo kutoka nje hasa nguo za watoto pamoja na kusafirisha kwenda soko la ukanda wa Afrika Mashariki na baadae eneo la ukanda wa SADC.

“Kwahiyo hii ni fursa nzuri kwetu kutumia masoko mawili kupeleka bidhaa zetu huko. Muione fursa hii ili katika kipindi hiki ambapo muwekezaji anajiandaa kuwekeza phase ya pili tuwe tumeshajiandaa,” amesema.

error: Content is protected !!