December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia ataka vita dhidi ya ugaidi kuwekewa mkazo

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amewataka makamanda wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kuijadili changamoto ya ugaidi na kuzidi kuimarisha weledi katika mapambano dhidi ya magaidi ili kuweza kukabiliana nao kikamilifu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Pia amesema mapambano dhidi ya tishio la ugaidi si suala la vyombo vya ulinzi na usalama peke yake bali linahitaji ushirikiano kutoka taasisi mbalimbali.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 15 Novemba, 2021 katika ufunguzi wa kikao cha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na makamanda wa Jeshi la Wananchi Tanzania cha mwaka 2021 kilichofanyiika katika ukumbi wa Ngombe Ligalo jijini Dar es Salaam.

Amesema taasisi mbalimbali zikiwemo vyombo vya habari na asasi za kiraia zinatakiwa kuwa na jukumu la kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa amani na amadhara ya kujihusisha na vitendo vya ugaidi.

“Dunia yetu kwa sasa inakabiliwa na tatizo jipya la kiusalama yaani ugaidi kwani hulka ya ugaidi mtu yeyote bila kujali rangi, umri, dini, itikadi, kipato anaweza kuwa mhanga wa ugaidi mifano ipo nanyi mnaijua.

“Naiweka changamoto hii mbele yenu wakati mjadili na hili na vyombo vingine vya usalama ndani ya nchi, niwatake mzidi kuimarisha weledi wenu katika mapambano na ugaidi ili tuweze kukabiliana nao kikamilifu,” amesema.

Aidha, amesema wajibu wake mkubwa ni kutafuta uwezo wa kifedha, nyenzo na fursa mbalimbali za ushirikiano ili kulinoa jeshi hilo na kulijengea uwezo katika kukabiliana na matishio mapya kama vile ugaidi, uharamia, uhalifu unaovuka mipaka.

“Nami niwaahidi kama Amiri Jeshi mkuu, nimeanza kusimamia hilo na nitalisimamia kikamilifu nione jeshi letu linakuwa imara zaidi, linaimarika zaidi na kufanya kazi zake kwa uweledi zaidi.

Aidha, amesema kwa sasa hali ya utulivu imerejea katika maeneo ya Mkoa wa Mtwara baada ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kuimarisha ulizi na kukabiliana na tishio la ugaidi.

Amesema kuwa kundi la kigaidi linalotoka katika Jimbo Cabo Delgado nchini Msumbiji lilifanya tishio hilo katika baadhi ya vijiji vya Mkoa wa Mtwara hivyo kufanya wananchi kuwa na hofu huku shughuli za kiuchumi na kijamii zikisuasua.

“Katika kipindi cha hivi karibuni, hali ya ulinzi na usalama wa mipaka yetu hususani kule Kusini ilihatarishwa na tishio la kuwepo kwa kundi la kigaidi linalotoka katika Jimbo Cabo Delgado nchini Msumbiji, kundi hili hujaribu kufanya mashambulizi katika vijiji vyetu vya Mtwara hali inayosababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali lakini Jeshi letu limekwenda na linakabiliana na hali hilo” amesema Amri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini na kuongeza

“Serikali imepeleka vikundi maalumu katika mpaka huo kwaajili ya kuimarisha ulinzi na usalama, hali iliyosaidia kuleta utulivu na kurejesha shughuli za uchumi na kijamii katika eneo hilo na kupunguza hofu iliyokuwepo” amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo amesema katika kipindi kifupi ambacho Rais Samia ameingia madarakani takribani miezi saba, amelifanyia Jeshi mambo makubwa ikiwemo kuidhinisha kupandisha vyeo kwa maaskari na maofisa waliostahili kupandishwa vyeo.

error: Content is protected !!