July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia ataka PF3 iondolewe kunusuru maisha ya watu

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan, ameshauri kifungu cha Sheria ya Jeshi la Polisi  kinachokataza majeruhi wa ajali kutibiwa hadi wapate Fomu ya Polisi ya Matibabu (PF3), kiondolewe ili kuokoa maisha ya watu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kiongozi huyo wa Tanzania ametoa wito huo leo Jumanne tarehe 18 Mei 2021, akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa Chuo cha Ushonaji cha Polisi Kurasini mkoani Dar es Salaam.

Rais Samia amesema watu wengi hupoteza maisha kutokana na kuchelewa kupata matibabu kufuatia kukosa fomu hiyo.

IGP Simon Sirro

“Suala la wanaopata ajali, wanaumia kwa viwango tofauti mwingine anaumia anapofika hospitali ahudumiwe haraka.  Lakini kwa sheria yetu hawezi kuhudumiwa mpaka iende  PF3, watu wanafia pale hospitalini,”  amesema Rais Samia na kuongeza:

“Mtu anapopata ajali wa naomuokota na kupaniki mbio hospitali, hawakumbuki kurudi polisi. Naomba hii sheria muiangalie kwamba mtu anapofikishwa hospitali apate huduma mambo mengine ya kipolisi yaendelee, tunapoteza watu kwa sababu ya kipengele kidogo cha PF3.”

error: Content is protected !!