November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia ataka mchango wa Bibi Titi uandikwe

Bibi Titi Mohammed

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan, ameagiza watafiti na waandishi katika fani za sayansi ya jamii, kuibua mchango wa Bibi Titi Mohamed, katika ukombozi wa Tanganyika kutoka kwa wakoloni. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Samia ametoa agizo hilo leo Jumamosi, tarehe 23 Oktoba 2021, katika maadhimisho ya kilele cha wiki ya Umoja wa Wanawake Tanzania ulio chini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), yaliyofanyika Rufiji mkoani Rufiji, ili kumuenzi Bibi Titi aliyezaliwa mkoani humo.

“Hivyo basi, nitoe rai kwa watafiti na waandishi katika fani ya sayansi ya jamii, kuandika kuhusu mchango wa mama huyu wa shoka katika siasa za ukombozi,” amesema Rais Samia.

Kiongozi huyo wa Tanzania, amesema mchango wa Bibi Titi katika kupigania uhuru wa Tanganyika, haijaandikwa vya kutosha.

“Mchango wa bibi huyu katika harakati za ukombozi wa mtu mweusi kutoka katika makucha ya wakoloni ni mkubwa, japo haujaandikwa vya kutosha. Tumesomewa kitabu kimeandikwa taarifa zake lakini wamesoma page mbili tu. Kwa hiyo haijaandikwa vya kutosha,” amesema Rais Samia.

Akielezea harakati za Bibi Titi, Rais Samia amesema enzi za uhai wake alikuwa chachu ya wanawake kushirki katika siasa za ukombozi wa Tanganyika, ambapo alishirikiana kwa karibu na Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyrere, kudai uhuru wa nchi hiyo.

“Hatuwezi kuzungumzia harakati za Mwalimu Nyerere kudai uhuru bila kutaja jina la Bibi Titi na hali ya ujasiri katika vuguvugu la kudai uhuru kwa kiasi kikubwa ilijengwa kwa ushahiwishi mkubwa wa bibi huyu,” amesema Rais Samia.

Rais Samia Suluhu Hassan

Aidha, Rais Samia amesema Bibi Titi alikuwa mwanamke wa kwanza kuanzisha vuguvugu la kudai haki za wanawake, kabla mapambano hayo hayajapamba moto katika mataifa ya magharibi.

“Sifa nyingine za bibi huyu alikuwa mwanamke mwenye msimamo na kujiamini, suala la jinsia halikumfanya akose kujiamini. Alikua mtu wa kufanya kile alichokiamini kiko sahihi hata ikibidi kutofautiana na watu wengine wakiwemo viongozi wa juu,” amesema Rais Samia na kuongeza:

“Tukio kubwa linalotukumbusha ujasiri huu, ni pale alipokataa kuunga mkono Azimio la Arusha na kuamua kuachia vyeo vyote alivyouwa navyo wakati huo na mengine kuendelea.”

error: Content is protected !!