
Uwanja wa Ccm Mkwakwani
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekitaka Chama cha Mapinduzi (Ccm), kukarabati viwanja vyake kwa kuweka nyasi bandia, mara baada ya kupunguzwa kwa kodi ya ongezeko la thamani (VAT), kuanzia mwaka ujao wa bajeti. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)
Samia ameyasema hayo leo tarehe 15 juni 2021, alipokuwa akizungumza na vijana jijini Mwanza katika mkutano wa hadhara.
Katika mkutano huo Rais Samia amesema kuwa sekta ya michezo inatoa ajira kubwa kwa vijana, na ndio maana serikali ilianzisha mfuko wa maendeleo ya michezo katika kusisaidia timu za taifa na kuponguza tozo kwa mnyasi bandia.
“Tumeanzisha mfuko wa maendeleo ya michezo ili kuziandaa na kuzisaidi timu zetu za Taifa kwenye michezo mbalimbali, na kwenye mwaka ujao wa fedha tumefuta tozo za nyasi bandia.”
Mara baada ya kusema hayo Rais Samia alitoa maagizo kwa kwa Ccm ambao wanamiliki viwanja vya michezo nchini kwa asilimia kubwa, kuhakikisha vinawekwa nyasi bandia au ikishindikana watafute wafadhariu kwa kuwa michezo ni ajira.
“Viwanja vingi vinamilikiwa na ccm, lakini hali yake hairidhishi niombe sana viwanja hivyo vitengenewa, viwekwe nyasi Bandai na namtaka katibu mkuu kuandaa mpango maalumu ya kuboresha viwanja hivyo na kama hamviwezi tafuteni wawekezaji.” Alisema Rais Samia
Aidha Rais Samia alitoa agizo kwa Waziri wa Habari utamaduni Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa kuhakikisha wanajenga shule za michezo (Academy) kila mkoa, kwa ajili ya kuendeleza vipaji kwa vijana.
“Shule za michezo (Academy) zijengwe kwenye mikoa tofauti tofauti ili kukuza vipaji kwa vijana.” Alisema Samia
More Stories
Injinia Hersi kuanza na uwanja Yanga
Sopu aibuka kinara wa mabao ASFC
Mgunda atoa tahadhari kwa Mayele kesho