Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia ataja sababu panga pangua viongozi wa Serikali
Habari za Siasa

Rais Samia ataja sababu panga pangua viongozi wa Serikali

Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania
Spread the love

 

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amesema kutoelewana miongoni mwa viongozi wa Serikali na wasaidizi wao ndiyo sababu kubwa ya kupangua safu ya uongozi katika wizara mbalimbali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Amebainisha hayo leo Jumatatu tarehe 27 Februari 2023 mara baada ya kuwaapisha viongozi wapya aliowateua jana wakiwemo Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makati Wakuu wa wizara mbalimbali.

Mkuu huyo wa nchi amesema atahakikisha panga pangua hiyo itakuwa ni ya mwisho inayotokana na kutoelewana kwa watendaji wao wakuu wa serikali.

Amesema endapo ikitokea tena kutoelewana kwa viongozi basi wote hawana budi kuondoshwa badala ya kupanguliwa na kwamba watateuliwa wengine wapya.

“Likijitikeza tena inamaana hamuwezani hamuwezi kufanya kazi kwahiyo wote mtakwenda kama ni Katibu Mkuna Naibu wake mtakwenda wote, Waziri na Naibu wake mtakwenda wote…nataka nikiwapanga mfanye kazi kwasababu sioni sababu ya kutokuelewana,” amesema Rais Samia

Amesema viongozi hao watapewa semina elekezi itakayofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 1 Machi 2023 ambapo watapewa maelekezo yakutosha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!