December 4, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia ataja lishe duni sababu matumizi ‘vumbi la kongo’

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema lishe duni ndiyo chanzo kikubwa cha uwepo wa watu wenye matatizo ya afya ya uzazi na kupelekea matumizi ya dawa na vyakula vinavyotajwa kusaidia wenye matatizo hayo ikiwemo supu ya pweza na ‘vumbi la kongo’. Anaripoti Jonas Mushi, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza leo tarehe 30 Septemba, 2022, katika hafla ya utiliaji saini mkataba wa usimamiaji shughuli za lishe uliofanyika jijini Dodoma, Rais Samia amesema hivi vijana wengi wanahaika linapokuja suala la afya ya uzazi na kuwataka watafiti kutafuta suluhu la tatizo hilo.

“Watoto balehe, embu tufanyeni tafiti kwanini wanakuwa na lishe mbovu kwanini kunakuwa na hizo gaps za kuwa na watoto ambao wapo vizuri kiafya wakike na wakiume, je ni masuala yaliyoingia ya mitindo, nataka niwe ‘six packs’ niwe ‘slim’ nataka sijui mbavu ikae hivi kwanini sasa,” amesema Rais Samia na kuongeza;

“Wakifika wakati wa kuja kuwajibika kuongeza jamii wanahangaika mara supu ya pweza mara nini…tuna tatizo na mnalijua mnalificha, fanyeni utafiti.”

Amesema kwasababu tatizo hilo limekuwa siri “linaumiza zaidi vijana wetu ndiyo unasikia mara hayo niliyataja, mara sijui udongo wa kongo lakini tatizo kubwa lipo kwenye lishe, tatizo letu ni lishe.”

Rais Samia amewataka watafiti nchini kutafuta namna ya kufanya ili kuweza kuwa na watoto “mashababi” watakaoweza kupata watoto wenye afya.

Amesema hali hiyo ikiachwa kuendelea hivyo inaweza kusababisha Taifa kukosa rasilimali watu kwa kuzalisha watu “goigoi” wasuioweza kuzalisha kwaajili ya taifa lao.

“Taifa litakuwa na watu ambao ni mzigo kwa taifa ni watu ambao hawatazalisha kwaajili ya Taifa haijulikani mume nani mke nani,” amesema Rais Samia.

error: Content is protected !!