Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia asema utumishi ulijengewa heshima ya woga
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia asema utumishi ulijengewa heshima ya woga

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema heshima ya utumishi wa umma iliyokuzwa katika awamu ya tano ilikuwa ya woga. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Jumamosi tarehe 2 Aprili Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma wakati wa hafla ya kuwaapisha viongozi wateule.

“Hali yetu ndani ya civil service si nzuri sana, tunasifiwa kwamba adjustments tulizofanya awamu ya tano kidogo zimekuza heshima, lakini heshima iliyokuzwa ni ya uoga kwasababu kulikuwa na Simba wa Yuda ambaye ukimgusa sharubu anakurarua hata hivyo haijakua vizuri, ” Rais Samia

Mkuu huyo wa nchi amesema heshima inayotakiwa “iwe ya moyoni kila mmoja awe na itikadi moyoni kwake kwamba mimi ni mtumishi wa Serikali majukumu yangu ni haya.”

Aidha amewataka kila mytumishi kuheshimu mipaka yake na kuepuka kuingilia mipaka ya mwingine, “kila mmoja aheshimu line ya mwenzie. Hicho tunakosa Serikalini.

“Unaangalia leo kila siku unasikia Waziri kaparurana na Katibu, Naibu hamuheshimu Waziri wake sijui nani kafanya nini, nafikiri kuna kitu tunakosa pahala.”

Amesema kutokana na hali hiyo kwa upande wa Serikali inakwenda kuimarisha chuo cha utumishi na chuo cha uongozi ili kutoa mafunzo kwa watumishi wa umma nchini.

Aidha amelitaka Baraza la Maadili kwenda kusimamia sheria na kurekebisha maadili kwa watendaji kazi nchini.

1 Comment

  • Kwanini basi ulinyamaza kimya? Si ungejiuzulu? Au unafiki?
    Pia mama tumia Kiwahili – acha kuchanganya lugha

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Jaji Biswalo aendelea kung’ang’aniwa fedha za ‘Plea Bargaining’, CUF wataka ajiuzulu

Spread the love  CHAMA cha Wananchi (CUF), kimemtaka aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka...

Habari za Siasa

Bunge labaini madudu mfumo ukusanyaji mapato, h’shauri tatu kikaangoni

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali...

Habari za Siasa

Mkuu wa wilaya ya Rungwe azindua vyumba sita vya madarasa vya thamani ya 64 mil

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu amezindua vyumba...

Habari za Siasa

Mbunge afurahia mabilioni ya Samia kutua jimboni

Spread the love  MBUNGE wa Igunga, Nicholas Ngassa ameishukuru Serikali kwa utekelezaji...

error: Content is protected !!