RAIS Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inaangalia hesabu zake kama zinarhusu kupandishwa kwa kima cha chini na mshahara na kusisitiza kuwa watumishi wataendelea kupandishwa vyeo na kupata maslahi yao mengine. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Ameyasema hayo katika mahojiano na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Azam Media, Tido Mhando, yaliyorushwa leo Jumatano tarehe 4 Mei katika kituo cha televisheni cha UTV.
Mkuu huyo wa nchi amesema mwaka jana Serikali ilichukua hatua kubwa katika kuhakikisha mishahara ya watumishi inaongezeka ikiwemo kupunguza kodi ya mshahara kwa asilimia moja, kufuta tozo kwenye marejesho ya mikopo ya elimu ya juu pamoja na kupandsisha watu madaraja.
“Tutaangalia mahesabu yetu mapato yakituonesha kwamba tunaweza kupandiha mishahara, tutapandisha,” amesema Rais Samia.
“Kupandisha mshahara ni lugha nyepesi, lakini kama ni jitihada za kuwapa wafanyakazi kipato tulizifanya mwaka jana, lakini kwasababu hatukutamka watu hawasemi na watu hawapongezi kwamba serikali imesamehe moja mbili tatu na sasa mshahara umeongezeka ni mpake upande pale useme kima cha chini shilingi hizi,” amesema.
Amesema kima cha chini kinaweza kutamkwa lakini kisisaidie kama ambavyo Serikali ilifanya mwaka jana.
Ameongeza katika bajeti ya sasa pia watafanya hivyo isipokuwa hawatapunguza kodi ya mshahara “itabaki ile ile asilimia nane lakini madaraja yatapanda na yale mambo yote yanayomfanya mfanyakazi mshahara wake uongezeke kidogo,”
Leave a comment