November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia arejea Tanzania

Spread the love

 

SAMIA Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania amemaliza ziara yake ya siku tatu nchini Misri na kurejea nchini mwake leo Ijumaa, tarehe 12 Novemba 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …(endelea).

Rais Samia aliyeondoka Jumatano ya tarehe 10 Novemba 2021 kwenda Cairo, Misri kwa mwaliko wa Rais wa nchi hiyo, Abdel Fattah Al Sisi.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, Rais Samia amepokelewa na viongozi mbalimbali akiwamo makamu wake, Dk. Philip Mpango.

Akiwa Misri, pamoja na mambo mengine alifanya mazungumzo na mwenyeji wake katika maeneo kadhaa ya ushirikiano kati ya Tanzania na Misri ikiwemo Nyanja za diplomasia, uchumi, siasa, elimu, utalii na huduma za kijamii.

Pia, Rais Samia na mwenyeji wake, walishuhudia utiaji saini wa mkataba mmoja na hati saba za makubaliano kati ya Tanzania na Misri.

error: Content is protected !!