Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia apangua mawaziri
Habari za Siasa

Rais Samia apangua mawaziri

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri, Kwa kuwahamisha mawaziri wawili. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Leo tarehe 1 Aprili 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus, Rais Samia amemhamisha aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na utawala Bora, kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).

Taarifa hiyo inasema kuwa , Mhagama anachukua nafasi ya George Simbachawene, ambaye Rais Samia amemteua kwenda katika wizara aliyotoka ya Wizara ya Nchi, Ofisi ya Nchi, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

“Uteuzi Huu umeanza tarehe 1 Aprili 2023 na mawaziri wateule wataapishwa tarehe 2 Aprili 2023, saa 3 asubuhi, Ikulu jijini Dar es Salaam,” imesema taarifa ya Yunus.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!