May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia apangua Ma-RAS, wapya 11

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, jana tarehe 29 Mei 2021, amefanya uteuzi na uhamisho wa Makatibu Tawala wa Mikoa (RAS). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Gerson Msigwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Msigwa, Rais Samia amewateua Makatibu Tawala wa Mikoa  wapya 11 na kuwahamisha tisa huku sita wakibaki katika vituo vyao vya kazi.

Taarifa ya Msigwa imewataja Makatibu Tawala wapya kuwa ni, Rodrick Mpogolo, aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi. Kabla ya uteuzi huo,  alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara.

Dk. Athuman Juma Kihamia, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha. Kabla ya uteuzi huo,  alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Mkoani Kilimanjaro.

Rais Samia amemteua Hassan Abbas Rugwa, kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam. Kabla ya Uteuzi huo, alikuwa Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Mkoani Lindi.

Dk. Fatuma Ramadhan Mganga, ameteuliwa  kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma. Kabla ya uteuzi huo, alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Mkoani Dodoma.

Pia, Rais Samia amemteua Mussa Ramadhan Chogello, kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita. Kabla ya uteuzi huo,  alikuwa Afisa katika Ofisi ya Rais.

Ngusa Dismas Samike, ameteuliwa na Rais Samia, kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza. Kabla ya uteuzi huo  alikuwa Katibu wa Rais, Ikulu.

Mhandisi Mwanaisha Tumbo, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Pwani. Kabla ya uteuzi huo, alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mkoani Tanga.

Hali kadhalika, Rais Samia amemteua, Doroth Aidan Mwaluko, kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida. Kabla ya Uteuzi huo,  alikuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu).

Balozi Batilda Salha Buriani, ameteuliwa  kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga. Kabla ya uteuzi huo, aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya na Japan.

Azza Hilal Hamad, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu. Kabla ya uteuzi huo, aliwahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga.

Rais Samia amemteua, Pili Hassan Mnyema,  kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga. Kabla ya uteuzi huo,  alikuwa Afisa katika Ofisi ya Rais.

Makatibu Tawala wa Mikoa waliohamishwa vituo vya kazi;

Rais Samia amemhamisha Dk. Seif Abdallah Shekillage, aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Amemhamisha, Karoline Albert Mthapula, aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara.

Rais Samia amemhamisha  Albert Gabriel Msovela, aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara.

Dk. Angelina Mageni Lutambi, aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, amehamishwa kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya.

Rais Samia memhamisha Mariam Amri Mtunguja, aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro.

Pia, amemhamisha Abdallah Mohamed Malela, aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara.

Aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Judica Haikase Omari, amehamishwa    kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa Njombe.

Rais Samia memhamisha, Denis Isdory Bandisa, aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa.

Aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Missaile Albano Musa, amehamishwa kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe.

Makatibu Tawala wa Mikoa wanaobaki katika vituo vyao vya kazi; Happiness William Seneda, anabaki kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa.

Prof. Faustine Kamuzora, anabaki kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera.

Rashid Kassim Mchatta, anabaki kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma.

Rehema Seif Madenge anabaki kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi.

Steven Mashauri Ndaki anabaki kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma.

Na Msalika Robert Makungu, anabaki kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora.

Taarifa ya Msigwa imesema, wateule hao wataapishwa katika Ikulu ya Chamwino, tarehe 2 Juni 2021.

error: Content is protected !!