Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia apangua baraza la mawaziri
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia apangua baraza la mawaziri

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri, kwa kuteua mawaziri na manaibu waziri wapya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Mabadiliko hayo yametangazwa leo Jumatano tarehe 31 Machi 2021, katika hafla ya uapisho wa Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk. Phillip Mpango.

Rais Samia amesema, mabadiliko hayo yamefanyika baada ya kumuondoa Dk. Mpango katika Wizara ya Fedha na Mipango.

“Kuondoka kwake wizara ya fedha kumeacha wazi baraza la mawaziri, natambua hilo kuna kazi inafanyika.”

“Tuko kwenye Bunge la Bajeti ambalo waziri wa fedha ni muhimu, nimesema nisifanye kazi kidogo kidogo hii imenipa sasa kulitazama baraza lote la mawaziri, nimefanya mabadiliko madogo,” amesema Rais Samia.

Mabadiliko hayo yameenda sambamba na uteuzi wa wabunge wa kuteuliwa na Rais, ambao ni Dk. Bashiru Ally, Balozi Liberate Mulamula na Balozi Mbaruku Nassoro Mbaruku.

Dk. Bashiru Ally

Dk. Bashiru, alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi na nafasi yake ameteuliwa Balozi Hussein Katanga, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan.

“Ndani ya baraza la mawaziri na nitalija baraza nililopanga hapa, zege halilai, lakini kabla sikuingia kwenye baraza, nimefanya uteuzi wa wabunge watatu, sasa uteuzi huu umenipeleka kufanya baraza la mawaziri,” amesema Rais Samia.

Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Ummy Mwalimu, amehamishiwa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, huku waliokuwa manaibu wa wizara hiyo wakiendelea kubaki.

Nafasi ya Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, ameteuliwa Mohamed Mchengelwa huku aliyekuwa anaishikilia, George Mkuchika, atapangiwa majukumu mengine.

Balozi Liberate Mulamula akiwa na Rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama

Seleman Jafo, aliyekuwa Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, amehamishiwa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, huku naibu wake akiwa Hamad Chande.

Pia, Wizara ya Uwekezaji imehamishwa kutoka Ofisi ya Rais kwenda Ofisi ya Waziri Mkuu huku waziri wake akiwa Geofrey Mwambe na naibu wake akiwa William Tate Ole Nasha.

Aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Mwigulu Nchemba, amehamishiwa katika Wizara ya Fedha na Mipango, naibu wake, Mhandisi Hamad Massauni.

Prof. Palamagamba Kabudi, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, amepelekwa Wizara ya Katiba na Sheria na msaidizi wake ni Joefrey Mizengo Pinda.

Profesa Palamagamba Kabudi

Balozi Liberate Mulamula, ameteuliwa kumrithi Prof. Kabudi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, huku naibu wake akiwa ni Balozi Mbaruku.

Mabadiliko hayo pia yamegusa Wizara ya Viwanda na Biashara, ambapo Rais Samia amemhamisha aliyekuwa Waziri wa Uwekezaji, Dk. Kitila Mkumbo, kwenda Wizara ya Viwanda na Biashara.

Pia, mabadiliko hayo yamegusa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kwenye nafasi ya naibu waziri.

Aliyekuwa naibu waziri wa wizara hiyo, Abdallah Ulega, ameplekwa kuwa naibu wizara ya Mifugo na Uvuvi, aliyokuwa akihudumu zamani huku Waziri wa michezo, Innocent Bashingwa, akibaki kwenye nafasi hiyo.

Abdallah Ulega

Nafasi ya Ulega kwenye michezo ameteuliwa Pauline Gekul, aliyekuwa naibu waziri wa mifugo na uvuvi.

Rais Samia amesema katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, amefanya mabadiliko kwa kuongeza naibu waziri mmoja, Mwanaidi Ally Hamisi. Waziri wake atabaki Dk. Dorothy Gwajima.

Kwa sasa kuna manaibu waziri wawili, Dk. Godwin Mollel ambaye anashughulikia masuala ya afya, na Mwanaidi akishughulikia maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto.

Rais Samia amesema baadhi ya wizara hakufanya mabadiliko, ikiwemo Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga, Mambo ya Ndani, Ujenzi na Uchukuzi, Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Maji na ile ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Wizara ya Madini, Maliasili na Utalii, Kilimo na Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Baada ya kutangaza mabadiliko hayo, Rais Samia amesema viongozi hao wataapishwa kesho Alhamisi tarehe 1 Aprili 2021, Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Mwigulu Nchemba

Kiongozi huyo wa Tanzania, amewataka mawaziri hao kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, huku akionya kuwaondoa watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao.

“Nimeona niwabadilishe, ni muda mfupi kuona nani kashindwa kafanya nini nimeona niwabadilishe. Tunakokwenda nataka kusema tunaanza na hao. Awamu ya sita inaanza na hao jinsi tunavyokwenda tutaona nani tunabaki naye. niwaombe mkafanye kazi zenu,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amepangua baraza la mawaziri kwa mara ya kwanza, tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Tanzania, tarehe 19 Machi 2021, akichukua mikoba ya Hayati Dk. John Magufuli, aliyefariki dunia tarehe 17 Machi 2021.

Dk. Magufuli alifariki dunia akiwa madarakani, kutokana na ugonjwa wa mfumo wa umeme wa moyo, na mwili wake ulizikwa nmyumbani kwao Chato mkoani Geita, tarehe 26 Machi 2021.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!