Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia aonya wanaofungulia chemba za vyoo barabarani, ataka Dar wabadilike
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia aonya wanaofungulia chemba za vyoo barabarani, ataka Dar wabadilike

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Watanzania na wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam kuacha tabia kufungulia chemba za vyoo kwenye mitaro ya barabara hali inayohatarisha afya za watoto pamoja na jamii kwa ujumla. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Pia amewaomba wananchi kutunza miundombinu inayojengwa kwani inatumia fedha nyingi hivyo itakapoharibiwa itaitia hasara serikali.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 5 Disemba, 2021 jijini Dar es Salaam wakati akizindua rasmi upanuzi wa barabara ya New Bagamoyo kutoka Morocco – Mwenge yenye urefu wa kilomita 4.3.

Amesema miradi hiyo inatakiwa kutunzwa kwa lengo la uboresha wa miundombinu hiyo ni kupunguza msongamano na kurahisisha usafiri na usafirisha wa bidhaa kwa maendeleo ya jamii husika na Taifa kwa ujumla.

Amesema ndani ya Dar es Salaam kuna mambo mengi yanatokea, kuna wananchi ambao hawaoni kwamba miradi hii ni fedha nyingi zinatumika hivyo inahitaji kutunzwa.

“Kuna watu ambao wanatupa taka na kuziba mitaro ile inayopitisha maji, hawajali kama mitaro itaziba, mvua kidogo zikinyesha wanafungulia vyoo vyao na kumiminika kwenye mitaro bila kujali watoto wetu wakati mwingine watundu… hawasikii wanaingia kwenye mitaro wanabeba maradhi.

“Lakini kuna wanaochimba michanga kwenye miundombinu ambayo imejengwa na kufanya miundombinu hiyo isiwe umadhubuti unaotarajiwa.

“Wapo wanaopaki magari pembeni na kuachia mafuta kufanya barabara zitaboke na zikitoboka ndio mwanzo wa ubovu, kuna tabia za ajabu ajabu zimekuwa zikifanyika, niombe sana na Tanzania nzima, tuende tukatunze miundombinu tunayojenga,” amesema.

Ameongeza kuwa miundombinu huwa inajengwa kwa umri kadhaa na pesa inayotumika kuweka barabara inakisiwa kwa umri kadhaa.

“Sasa tunapoharibu tunaitia hasara serikali kurudia kutengeneza na umadhubuti wa ile miundombinu unaathirika, kwa hiyo niombe sana tubadilike, tuendeni na kasi ya maendeleo jinsi yanavyoletwa, tupokee miradi tuitunze jinsi ipasavyo. Nawasihi sana kuzingatia sheria ili kupata manufaa yaliyokusudiwa,” amesema

Awali akitoa taarifa kuhusu mradi huo, Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Rogatus Mativila amesema upanuzi wa sehemu hiyo ya New Bagamoyo unalengo la kupunguza wa magari mengi yanayoingia na kutoka katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Muonekano wa barabara ya Mwenge-Morocco

“Ili lengo hili la kupunguza msongamano wa magari litimie na magari yaweze kutembea bila kusimama simama, usanifu wa barabara hii umezingatia kupunguza muingiliano ya moja kwa moja kwenye huduma mbalimbali zilizo karibu na barabara kama ilivyofanyika kwenye awamu ya kwanza iliyojengwa ya Mwenge -Tegeta.

“Upanuzi wa sehemu hii ya barabara ni awamu ya pili baada ya awamu ya kwanza kukamilika kati ya Mwenge –Tegeta kibaoni yenye urefu wa kilomita 12.7 ambayo ilijengwa kwa fedha za msaada wa Wakala wa Ushirikiano wa Kimaitafa wa Japana – Jica. Awamu ya kwanza ilikamilika mwaka 2015.

“Amesema awamu zote mbili zinafikisha kilomita 17 kutoka Morocco hadi Tegeta Kibaoni.

Ameongeza kuwa awamu hiyo ya pili pia inafadhiliwa na fedha za JICA sawa na Sh bilionio 71.8.

“Serikali ya Tanzania imechangia kutoa msamaha wa tozo mbalimbali stahiki katika utekelezaji wa mradi ambayo unahusisha uhamishanji wa miundombinu pamoja na fidia yenye jumla ya Sh bilioni 8.2.

“Barabara imepanuliwa kwa kujenga njia nne zenye urefu wa mita 3.52 kwenda kila upande. Katika barabara kumetengwa eneo la upana wa mita tisa kwa ajili ya mradi wa mabasi ya usafiri wa haraka BRT, barabara mbili kila upande,” amesema.

1 Comment

  • Ni kweli mama.
    Sheria za matumizi sahihi ya barabara zinasimamiwa na Polish wa trafiki.
    Mbona hawatoi faini?
    Je, kwanini barabara hii, Morogoro Road, Pugu na Ile ya Mwenge mpaka Pugu zisisimamiwe na Polisi Kanda Maalum, Dar-es-salaam?
    Halafu, Polisi wa Kanda zingine wasimamie barabara za Kanda zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

error: Content is protected !!