Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Kitaifa Rais Samia aonya polisi kukamata watu kwa vitisho, kutia hofu
Kitaifa

Rais Samia aonya polisi kukamata watu kwa vitisho, kutia hofu

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan amewataka polisi kutowakamata wananchi kwa vitisho, wala kuwatia hofu kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume na misingi na kiapo cha jeshi hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu…  (endelea)

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 12 Desemba, 2021 wakati wa kufunga mafunzo ya kozi ya uofisa kutoka Chuo cha Maofisa wa Polisi Dar es salaam.

Katika mafunzo hayo, jumla ya maofisa ukaguzi 747 wamehitimu kozi hiyo na kupangiwa vituo vya kazi.

Amesema wanapokwenda kumkamata mtu hawatakiwi kufanya vitisho.

“Lakini huko mtaani tunaona kabisa ni vitisho, harassment, wakati mwingine mtu anakamatwa bila kosa la maana. Umekerana na bosi wa askari, anaamua kukutia adabu, lakini kuna tuhuma za rushwa kwa askari wa polisi, hili ni katazo lipo hata kwenye ile nyimbo yenu.

“Nyingine tunaona kwenye viclip vinavyorushwa… askari kabisa ana-bargain kwenye gari ya mtalii apewe pesa bila kujua mtalii ana kalamu inamrekodi. Askari wanavunja sheria pamoja na kwamba askari ni msimamizi wa sheria, baadhi yenu ambao hawakuiva kimaadili ndio wanavunja sheria,” amesema Rais Samia.

Amesema askari wengine wanatokwa na uaminifu wanachota mali za watu, mali za serikali… vitendo vyote hivyo halivijengi vizuri Jeshi la Polisi.

Amesema mambo hayo yanatokea labda kwa sababu wamechelewa kuwapeleka mafunzo au hawajahitimu vizuri.

“Niliwahi kumuuliza IGP, huko kwenye mafunzo yenu kuna watu wanashindwa kozi kweli? Mbona wanapoenda Moshi wanarudi wote, akanijibu kuna mafunzo wanafaulu wote, najiuliza wanafaulu wote hivi! Askari anaingiza kichwa ndani ya gari!

Aidha, Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Simon Sirro naye aliwaonya wanaojipanga kufanya uhalifu wa kutumia silaha katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka kwa kigezo cha kutafuta fedha.

Sirro amesema wapo macho, “tunapokaribia sikukuu za mwisho wa mwaka wale ambao silaha zao wamezificha wanaamua kuingia barabarani kutafuta fedha.”

“Sasa niwaombe sana Watanzania tumalize mwaka vizuri. Huna sababu ya kuingia kwenye makosa haya ya bunduki unatisha Watanzania bila sababu na kujiweka maisha yako hatarini.”

Aidha amesema hali ni shwari ingawa bado kuna matukio ya uhalifu.

Pia amekiri kuwepo kwa changamoto ya uhalifu wa makosa yanayovuka mipaka ni yale yanayoashiria ugaidi, usafirishaji dawa za kulevya na binadamu.

Hata hivyo, amesema wameweka mikakati kadhaa ikiwemo kutoa elimu kwa wananchi, kushirikisha viongozi wa vijiji, mitaa, kata na shehia katika doria za mitaani na kuanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi.

Pia kufanya doria za kawaida na doria maalum kuwasaka wahalifu na kuwashughulikia pamoja na kupunguza ucheleweshaji wa upelelezi ambako kesi kubwa upelelezi wake hautakiwi kuzidi mwaka na kesi ndogo miezi sita.

Akizungumzia mafunzo hayo Mkuu wa Chuo cha Maofisa wa Polisi Dar es salaam, SACP Lazaro Mambosasa amesema jumla ya wanafunzi 747 wamehitimu kozi ya Uofisa ‘gazetted officer’ kati ya wanafunzi 756 waliojiunga na kozi hiyo tarehe 18 Juni mwaka huu.

“Wanafunzi wametoka mikoa yote ya Tanzania bara na Visiwani. Wapo wenye elimu ya Shahada ya uzamivu (2), shahada ya uzamili (109), shahada ya kwanza (454), stashahada wapo 83, astashahada wapo 36. Jumla ni 684 sawa na asilimia 91.32 ya wanafunzi wote.

“Idadi ndogo iliyobakia wanafunzi 65 ambao ni asilimia 8.68 nao wana elimu ya kidato cha sita, nne na darasa la saba pamoja na uzoefu wa muda mrefu na sifa za kiutendaji ambazo zimewastahilisha kupata mafunzo tajwa,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariKitaifa

Mabasi ya New Force yapigwa kitanzi kisa ajali

Spread the loveMAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), imefuta ratiba za safari...

HabariKitaifa

Spika Tulia aeleza sababu za kengele ya hatari kulia Bungeni

Spread the loveSPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, amesema kengele ya hatari...

HabariKitaifaTangulizi

Ni Bajeti ya kulipa madeni, mzigo wa kodi

Spread the love WAZIRI wa fedha, Mwigulu Nchemba, amewasilisha bajeti ya serikali...

Kitaifa

Serikali yatenga eka 10 kwa kila kijana mwenye sifa kufanya kilimo

Spread the love  SERIKALI nchini Tanzania imetenga eka 10 kwa kila kijana...

error: Content is protected !!