Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Rais Samia aokoa wanafunzi 271 kutoka ‘zizini’
ElimuHabari

Rais Samia aokoa wanafunzi 271 kutoka ‘zizini’

Spread the love

JUMLA ya Sh milioni 40 zilizotolewa na Serikali kupitia mkopo nafuu wa mapambano dhidi ya Uviko-19 zimeweka historia kwa wanafunzi 271 wa Shule Shikizi ya Mwamashiga iliyopo Uyui mkoani Tabora baada ya kujengewa madarasa ya kisasa na kutoka kwenye ‘zizi’. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hatua hiyo imekuja ndani ya mwaka mmoja baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuingia madarakani na kufanikisha kupatikana mkopo nafuu wa Sh trilioni 1.3 kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF) ambazo zimetumika katika maboresho kwenye sekta ya elimu na afya nchini.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi na wanafunzi wa Mwamashiga, wamesema walipoanza kusoma katika madarasa hayo ya nyasi, awali yalionekana kama zizi.

Mmoja wa wanafunzi hao Mathias Kasenga, Mwanafunzi pia hapakuwa na madawati bali walikaa kwenye mabenchi.

Aidha, Mlezi wa Shule hiyo, Zahran Salehe amesema Shule ya Mwamashinga ilianza katika mazingira ya shule shikizi ikilelewa na shule mama ambayo ni Shule ya Msingi Katunda.

Amesema wanafunzi walikuwa wanasoma katika madarasa ya nyasi kwa miaka mingi.

Amesema wanafunzi waliokuwa wanasoma katika Shule hiyo walikuwa wanatembea umbali wa zaidi ya Kilomita 120 kutoka makao makuu ya wilaya ya Halmashauri Uyui mkoani Tabora.

“Disemba mwaka jana, tulijenga madarasa mawili kutokana na fedha za Uviko-19, tulipewa Sh milioni 40 ambazo pia tulitumia kujenga vyoo matundu 12 ya kisasa,” amesema.

“Watoto wa eneo hili walikuwa hatarini kwa kutembea umbali wa Kilomita 120 kwenda na kurudi kufuata elimu ya msingi, lakini sasa Hangaya iliyo nyota ya asubihi imewawakia,” amesema Liberatha Mbeshi ambaye ni mkazi wa Mwamashiga.

Mbeshi ameongeza kuwa wanafunzi sasa wanasoma vizuri, hivyo anaishukuru serikali kwani wamewaletea pia walimu wanne.

“Tulipata msaada nafikiri hata kabla Rais Samia hajamaliza mwaka madarakani lakini akatupatia madarasa haya, tunaomba aongeze juhudi zaidi,” amesema.

Zaidi ya wanafunzi 271 wanaosoma katika shule hiyo sasa wamepunguziwa umbali wa kutembea kilomita 120 na sasa baadhi wanatembea umbali wa kilomita mbili au tatu.

Pia wanafunzi hao wametoka kwenye madarasa ya nyasi kwenda kwenye madarasa ya kisasa na shule hiyo sasa ni shule kamili sio kituo shikizi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanawake GGML wawanoa wanafunzi Kalangalala Sec. kujitambua

Spread the loveKATIKA kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, Umoja wa...

error: Content is protected !!