Saturday , 3 June 2023
Home Kitengo Michezo Rais Samia anunua tiketi 5000 Yanga vs USM Alger
Michezo

Rais Samia anunua tiketi 5000 Yanga vs USM Alger

Spread the love

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amejitoa kimasomaso kuhakikisha kuwa Yanga inashinda nyumbani dhidi ya USM Alger ya Algeria kwa kununua tiketi 5000 ili mashabiki waingie uwanjani. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mechi hiyo ya fainali inayosubiriwa kwa hamu imepangwa kupigwa tatehe 28 Mei 2023 katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni mechi ya mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Mei 2023 Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema tiketi hizo ni mwendelezo wa kuongeza hamasa, ikiwa ni baada pia ya kuahidi Sh 20 milioni kila bao la ushindi litakalofungwa na wachezaji wa Yanga kwenye mechi hizo za fainali.

“Rais Samia anahakikisha kuwa Yanga inachukua Kombe kwa kuendeleza hamasa hizi za kununua tiketi 5000 kwa lengo la kuujaza uwanja wa Taifa utakaoshuhudia mchezo mgumu wa fainali kati ya timu ya Tanzania dhidi ya USM Alger.

“Rais anawataka Watanzania waende kuujaza uwanja wa Taifa, kwa sababu mama hana mbambamba katika mbio za Yanga kuitangaza nchi kimataifa kupitia mpira wa miguu,” Amesema.

Katika hatua nyingine, Msigwa aliwataka wachezaji kuingia uwanjani kwa nguvu zote ili washinde magoli mengi kwa sababu fedha za Rais zinazotolewa ili kuibua hamasa bado zipo kwa lengo moja la kuhakikisha Yanga inaibuka kidedea katika mechi zake za fainali za Kombe la Shirikisho.

Mechi ya marudiano kati ya Yanga na USM Alger inatarajiwa kupigwa nchini Algeria, Juni 6 mwaka huu, huku timu ya Tanzania ikiingia fainali kwa mara ya kwanza katika historia ya michuano ya Kimataifa inayoendeshwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika.

Fiston Mayele mshambuliaji maya wa Yanga

Mengine makubwa yaliyofanywa na Rais Samia dhidi ya Yanga katika mechi yao ya fainali ni kuipa ndege klabu hiyo ili iende Algeria katika mechi yao ya marudiano.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Dk. Mkwizu: Afrika tudumishe utamaduni

Spread the love  MWENYEKITI wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Mkoa wa...

Michezo

‘EONII’ kuteka tasnia ya filamu

Spread the love  UZINDUZI wa Filamu ya Kisayansi ya ‘EONII’ uliofanyika Mei...

Michezo

NBC Dodoma Marathon yazinduliwa, wakiambiaji 6,000 kushiriki

Spread the loveBENKI ya NBC imetangaza kufanyika kwa mbio kubwa za NBC...

Michezo

Mwenyekiti UVCCM anogesha nusu fainali Kimwanga CUP, Hawa Abdul Rede CUP kwa kishindo

Spread the loveHEKAHEKA za michuano ya kuwania kuingia fainali ya michuano ya...

error: Content is protected !!