Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari Rais Samia anavyoifunga Tanzania, uwekezaji na mauzo yapaa
HabariTangulizi

Rais Samia anavyoifunga Tanzania, uwekezaji na mauzo yapaa

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania imesema ziara za mkuu wa nchi hiyo Rais Samia Suluhu Hassan nje ya nchi zimeongeza uwekezaji wa ndani kwa kufikia dola bilioni 9 (Sh.20 trilioni) na mauzo ya nje yamefikia dola bilioni 10 (Sh.23 trilioni). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo yamesemwa leo Jumanne tarehe 28 Juni 2022 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Uviwanda na Biashara, Profesa Godius Kahyarara, Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia mafanikio ya ziara za Rais Samia na Filamu ya Royal Tour.

Profesa Kahyarara amesema, katika utawala wa Rais Samia amewezesha kuifungua nchi kiuchumi, “mauzo yetu ya nchi yalikuwa yanafikia Dola bilioni 7 hadi 8 lakini sasa tumefikia dola bilioni 10 ni jambo kubwa.”

“Tangu Rais aliposema sasa anaifungua nchi yaani Machi mwaka jana hadi sasa, uwekezaji wetu wa ndani umefikia zaidi ya Dola bilioni bilioni 9. Hii ni kwa kuangalia vigezo mbalimbali na imechangiwa na ziara na sera za serikali anayoingoza,” alisema

Aidha, katibu mkuu huyo amesema, wamefuatilia kuona utendaji wa hoteli mbalimbali ambazo zilifungwa kabla na baada ya UVIKO-19 ili kuona kilichowafanya wakazifunga.

“Katika muda mfupi hoteli zote zilizokuwa zimefungwa tuliangalia kwa nini zilifunguliwa na kwa sasa zinafunguliwa kwa wingi na kwa Dar es Salaam hoteli nyingi zimeanza kufunguliwa sana na sababu kuwa ni msukumo wa The Royal Tour,” alisema

Profesa Kahyarara alisema alisema, ziara za Rais Samia zimeendelea kuwavitua wawekezaji mbalimbali,”na naweza kusema kuna mwekezaji anataka kuwekeza
Kwenye hotel katika maeneo kama Serengeti. Zanzibar, Arusha na Mwanza.”

Amesema, mwekezaji huyo yupo hatua ya kufikia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), “na karibia anapewa maeneo ya uwekezaji na wiki chache zijazo mtamfahamu.”

Awali, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu ya Tanzania, Zuhura Yunus amesema, ziara ya Rais Samia nchini Oman imekuwa na mafanikio makubwa baina ya mataifa hayo mawili.

Zuhura amesema, Rais Samia akiwa Oman alishuhudia makubaliano mbalimbali yakiingiwa baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Oman na kamapuni binafsi kwenye nyanja za elimu, mifugo, nishati na usafirishaji ambayo ni fursa adhima kwa nchi kuchochea ukuaji wa uchumi.

Kwa upande wake, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amesema, wizara hiyo iliingia makubaliano na kampuni moja ya Oman ambayo wanatarajia kuongeza mauzo ya nyama na fedha za kigeni.

Ndaki amesema, makubaliano hayo yatasaidia kampuni za Ranchi ya Taifa kununua mifugo mingi kwani itakuwa na uwezo wa kuuza wanyama hai kuwapeleka Oman na wafugaji wataongeza kipato kwa kuuza wanyama wao kwa Kampuni Ranchi ya Taifa.

“Kampuni za Oman zitakuja kuwekeza hapa nchini kwa mazao ya kuchakata nyama na ujio wao utaongeza ajira kwa vijana wa Kitanzania na fedha za kigeni,” amesema

Aidha, waziri huyo amesema Rais Samia alimruhusu kwenda Saudia kuzungumza kuhusu kuanza kupeleka nyama huko ambako kulizuiwa na soko hilo liko tayari.

“Sasa tunaruhusa ya kupeleka nyama kule Saudia na tunamshukuru sana Rais kwa sababu yeye alinipa kibali kwenda Saudia kuzungumza nao kuona namna ya kuondoa zuio lililokuwepo,” amesema Ndaki

“Tumejipanga kudhibiti magonjwa na kufikia vigezo vinavyotakiwa ili kutuwezesha kuuza nyama nje. Saudia ni kama miaka 21 walituzuia na sasa tuna zoezi la kutambua na kusajili mifugo yetu nchi nzima ili kuwa na nyama yenye viwango,” alisema

Naye Waziri wa Nishati, January Makamba amesema, makubaliano waliyoingia ni baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Oman yenye lengo la kujengeana uwezo, kwenye maeneo mbalimbali, kubadilishana wanafunzi kutoka hapa kwenda kule naweza kusema nim, “ni mwamvuli mnapa wa mahusiano baina ya serikali hizi mbili.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!