May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia anahutubia Bunge

Samia Suluhu Hassani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Spread the love

 

SAMIA Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania, leo Alhamisi kuanzia saa 10:00 jioni, atalihutubia Bunge la nchi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Rais Samia, analihutubia Bunge kwa mara ya kwanza, tangu alipoingia madarakani tarehe 19 Machi 2021, akichukua nafasi ya Hayati John Pombe Magufuli, aliyefariki dunia.

Hayati Magufuli, alifariki dunia tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena, Makumbusho mkoani Dar es Salaam na mwili wake kuzikwa nyumbani kwao, Chato mkoani Geita.

Rais Samia anakwenda kulihutubia Bunge hilo, ambalo Hayati Magufuli alilizindua tarehe 13 Novemba 2021.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

error: Content is protected !!