RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan Yusuf Tindi Mndolwa kuwa Balozi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Mdolwa, ameapishwa leo Jumatatu, tarehe 19 Aprili 2021, Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali, akiwemo Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango.
Mdolwa aliteuliwa juzi Jumamosi kuwa Balozi na akamteua pia kuwa Mkuu wa Itifaki (Chief of Protocol) katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Pia, Rais Samia alimteua Benedict Ndomba kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA).
Kabla ya uteuzi huo, Ndomba alikuwa Mkurugenzi wa Miundombinu na Operesheni wa eGA na anachukua nafasi ya Dk. Jabir Bakari Kuwe ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Wateuliwa hao, wamekula kiapo cha uaminifu kwa viongozi wa umma, kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili, Jaji Sivangilwa Mwangesi.
Leave a comment