Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia amwandikia ujumbe Rais Mwinyi
Habari za Siasa

Rais Samia amwandikia ujumbe Rais Mwinyi

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

JANA Jumanne, tarehe 2 Novemba 2021, Dk. Hussein Ali Mwinyi alitimiza mwaka mmoja tangu alipoapishwa kuwa Rais wa nane wa Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Aliapishwa na aliyekuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othuman Makungu katika Uwanja wa Aman kuchukua nafasi ya Dk. Ali Mohamed Shein aliyemaliza muda wake wa utawala wa miaka kumi kwa mujibu wa Katiba.

Kwa sasa Makungu ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania.

Leo Jumanne, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametumia ukurasa wake wa Twitter, kuzungumzia mwaka mmoja wa utawala wa Rais Mwinyi.

Ameandika “Nakupongeza Mhe. Rais @DrHmwinyi kwa kutimiza mwaka mmoja tangu uingie madarakani kuwa Rais wa Nane wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Wazanzibar tuna imani na wewe na tunakutakia kheri katika kuijenga Zanzibar bora. Nakuahidi ushirikiano zaidi.

Yeye mwenyewe, Rais Mwinyi alitumia ukurasa wake wa Twitter kuzungumzia uongozi wake wa mwaka mmoja akisema “ni mwaka mmoja tangu nimeingia madarakani. Namshukuru Mwenyezi Mungu na wananchi wote wa Zanzibar kwa kunichagua. Tuzidi kuendeleza mashirikiano baina yetu na kuilinda tunu ya Umoja, Amani na Utulivu tulionao. Safari ya Ujenzi wa Uchumi Mpya inaendelea.”

1 Comment

  • MWAKA MMOJA SASA KIONGOZI ALIYECHAGULIWA NA VIFARU PAMOJA NA MITUTU YA BUNDUKI UKISEMA UCHUMI WA “BLOU” UNAKAMATWA, HAPO NDIO WA ZANZIBARI TUAMKE HAKUNA MPYA NDIO WALE WALE WALIOSEMA ZANZIBAR ITAKUWA KAMA DUBAI MATOKEO YAKE HATA (BAIT AJAB) LIMEPOROMOKA ACHENI KUCHEZA NA AKILI ZA WANZANZIBAR HATUTOCHOKA KUDAI MAMLAKA KAMILI YA NCHI YETU.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!