August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia amteua Mkuu mpya wa majeshi

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Meja Jenerali Jacob Mkunda kuwa Jenerali na kumteua kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi(CDF). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma …  (endelea).

Kabla ya uteuzi huo Mkunda alikuwa Mkuu wa Tawi la Operesheni na Mafunzo makao makuu ya jeshi.

Jenerali Mkunda anachukua nafasi ya Jenerali Venance Mabeyo ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria.

Katika hatua nyingine Rais Samia amempandisha cheo Meja Jenerali Salum Haji Othman kuwa Luteni Jenerali na kumteua kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania. Kabla ya uteuzi huo Meja Jenerali Othman alikuwa Kamishna wa Utafiti na Maendeleo jeshini katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kuhenga Taifa.

Jenerali Venance Mabeyo, Mkuu wa Majeshi Tanzania anayemaliza muda wake

Meja Jenerali Othman anachukua nafasi ya Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule ambaye ameteuliwa kuwa balozi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Alhamisi tarehe 29 Juni, 2022 na Mkurugenzi wa Mawsiliano ya Rais Ikulu Zuhura Yunusi, uapisho wa wateule hao utafanyika kesho Ijumaa tarehe 30, Juni, 2022 Ikulu jijini Dar es Salaam.

error: Content is protected !!