Sunday , 26 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia amsimamisha DC Sabaya, ateua
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia amsimamisha DC Sabaya, ateua

Lengai Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai
Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemsimamisha kazi Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazomkabili. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). 

Taarifa ya Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu imesema, Sabaya amesimamishwa kazi kuanzia leo Alhamisi tarehe 13 Mei, 2021.

Wakati huo huo, Rais Samia amemteua Nsubili Akomeligwe Kajela Joshua kuwa Karani wa Baraza la Mawaziri. Joshua alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Rais Samia amemteua, Ayub Musa Makoye kuwa Naibu Karani wa Baraza la Mawaziri. Makoye alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Katika hatua nyingine, Rais Samia amemteua Dk. Stergomena Tax kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute). Dk. Tax ni Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Rais Samia amemteua Dk. Laurian Ndumbaro kuwa Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Uongozi. Dk.Ndumbaro ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Sambamba na uteuzi huo, Rais Samia amefanya uteuzi wa wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya Uongozi ambao ni Balozi Riitta Swan, Prof. Penina Mlama, Lina Soiri, David Walker, Suzan Mlawi, Dk.Hamis Mwinyimvua na Prof. Samwel Wangwe.

Uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe 13 Mei, 2021.

Katika hatua nyingine, Rais Samia amemteua Ishmael Andulile Kasekwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).

Uteuzi wa Kasekwa umeanza tarehe 10 Mei, 2021 na amechukua nafasi ya Dk. Rosebud V. Kurwijila ambaye amemaliza muda wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!