May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia amsifu Dk. Magufuli, amtaja Dk. Kikwete, Karume

Spread the love

 

RAIS WA Tanzania, Samia Suluhu Hassa, amesifu uongozi wa kutukuka wa mtangulizi wake, Hayati John Magufuli huku akimtaja Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Amani karume kwamba ndiye aliyemuibua. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea).

Akihutubia Bunge leo tarehe 22 Aprili 2021, Rais Samia amesema, mtangulizi wake (Dk. Magufuli), alikuwa kiongozi bora, jasiri na aliyetumikia Taifa lake kwa dhati.

“Dk. Magufuli alikuwa kiongozi hodari, jasiri, shupavu na mwenye maoni ambaye aliipenda nchi yetu na kuitumikia kwa uadilifu mkubwa,” amesema.

Amesema, anashukuru chama chake – Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kumwamini na kwamba, kutokana na chama hicho, amekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amemtaja Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Aman Karume kwamba ndiye aliyemuibua na kumpa nafasi ndani ya serikali yake. Na kwamba, baada ya hapo, Dk. Jakaya Kikwete ambaye ni Rais Mstaafu wa Tanzania alimteua uwaziri pia Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba.

“Nimshukuru Rais Kikwete ambaye alinipa malezi haya, namshukuru kwa kunipa uwaziri katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano na kuniamini katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba.

“Namshukuru Dk. Magufuli kwa kuniamini na kuwa mgombea mwenza wake kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na 2020, kuniamini kwake kumeniwezesha kuwa mwanamke wa kwanza nchini kushika wadhifa wa kamamu wa rais na sasa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema.

error: Content is protected !!