October 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia ampongeza mshindi wa Nobel aliyejinyakulia bilioni 2

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

SAMIA Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania, amempongeza, Abdulrazak Gurnah kwa kutwaa tuzo ya amani ya Nobel katika fasihi 2021, kutokana na kuangazia suala la ukoloni na athari zake katika utunzi wake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Gurnah (73) ambaye ni Mwandisi wa riwaya nchini Tanzania alitangazwa mshindi jana Alhamisi, tarehe 7 Oktoba 2021 na Kituo hicho kinachotoa tuzo hizo za Nobel.

Profesa huyo wa fasihi ametwaa tuzo hiyo iliyotolewa na kituo hicho cha Sweden ina thamani ya corona milioni 10 za taifa hilo sawa na Sh bilioni 2.6.

Mara baada ya kutangazwa mshindi, Rais wa Tanzania, Samia ametumia ukurasa wake wa twitter kumpongeza mwana fasihi huyo.

“Nakupongeza Bw. Abdulrazak Gurnah kwa kutunukiwa Tuzo ya Nobel katika fasihi ya mwaka 2021. Tuzo hii ni heshima kwako, Taifa letu la Tanzania na Afrika,” ameandika Rais Samia

error: Content is protected !!