May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia ampagawisha Zuchu

Spread the love

 

Malkia wa Bongofleva, Zuhura Kopa maarufu kama Zuchu ameeleza kupagawishwa na simu ya Rais Samia Suluhu Hassan wakati akiperfome jana tarehe 21 Agosti, katika tamasha la ‘Zuchu Home Coming’ lililofanyika katika visiwa vya Unguja huko Zanzibar.Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Akipiga stori ya Mwanahalisi online baada ya kumalizika kwa tamasha hilo, Zuchu amesema simu hiyo ya Rais Samia ilimuonesha upendo wa kipekee na kuamiani kuwa Serikali inamuunga mkono yeye na wasanii wengine.

Rais Samia Suluhu Hassan

Aidha, akizungumzia tamasha hilo Zuchu amesema hakuamini kama anapendwa kiasi hicho kwa sababu tiketi hadi za VIP ziliisha siku tatu kabla ya tamasha kiasi cha kumlazimu kuongeza tiketi nyingine na kuvuka malengo ya idadi ya watu waliokuwa wanatakiwa ukumbini kwa mujibu wa masharti ya Corona.

“Hakika maandalizi yalikuwa makubwa maana sikua nalala, baada ya hii shoo ndio nitalala,” amesema.

Amesema licha ya wasanii wenzie wa lebo ya WCB kuwa bize na ratiba zao, mmoja wao Mbosso alionesha upendo wa dhati na kwenda kumuunga mkono katika tamasha hilo.

error: Content is protected !!