July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia amlilia kaka yake Mbowe

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzania nchini humo-Chadema kufuatia kifo cha kaka yake, Charles Mbowe. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Charles amefikwa na mauti usiku wa kumakia leo Jumatano, tarehe 8 Julai 2021, katika Hospitali ya KCMC, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Rais Samia ametumia ukurasa wake wa Twitter kutuma salamu za rambirambi akisema “Nakupa pole Ndg. Freeman Mbowe (Mwenyekiti wa CHADEMA) na wafiwa wote kwa kuondokewa na ndugu yenu mpendwa Charles Mbowe.”

“Nawaombea moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki cha majonzi. Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe, Amina,” amesema Rais Samia

Mapema leo Alhamisi mchana, Freeman amesema, kaka yake atazikwa nyumabani kwao Machame, Jumatatu tarehe 12 Julai 2021.

error: Content is protected !!