Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari Rais Samia amlilia balozi aliyefariki ajalini
HabariTangulizi

Rais Samia amlilia balozi aliyefariki ajalini

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine Mushy, kilichotokea katika ajali ya gari iliyotokea usiku wa Jumanne, maeneo ya Mkata, wilayani Handeni, Mkoa wa Tanga. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Dk. Samia ametuma salamu hizo za rambirambi leo Alhamisi, tarehe 15 Desemba 2022, kupitia ukurasa wake wa Twitter.

“Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Balozi Celestine Mushy Balozi wa Tanzania nchini Austria na Mwakilishi wa Kudumu wa nchi yetu katika Mashirika ya Kimataifa, Vienna. Tumeondokewa na mwanadiplomasia mahiri na mtumishi makini wa umma. Mungu amweke mahali pema. Amina,” ameandika Rais Samia.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Siriel Mchembe, Balozi Mushy alifariki dunia akiwa safarini kuelekea mkoani Kilimanjaro, akitokea jijini Dar es Salaam.

Marehemu Balozi Mushy aliteuliwa na Rais Samia kuiwakilisha Tanzania nchini Austria, Januari 2022.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!