May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia amlilia Askofu Mwenisongole, kuzikwa Desemba 30

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa salamu za pole kufutia kifo cha Askofu Mkuu mstaafu wa Tanzania Assemblies of God (TAG), Mchungaji Ranwell Mwenisongole. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Askofu Mwenisongole aliyekuwa Mchungaji Kiongozi wa TAG Upanga Jijini Dar es Salaam, alifikwa na mauti jana Jumamosi, tarehe 25 Desemba 2021.

Leo Jumapili, Rais Samia ametumia ukurasa wake wa Twitter kuzungumzia kifo hicho akasema,”nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Askofu Dkt. Ranwell Mwenisongole aliyekuwa Askofu Mkuu wa Awamu ya Pili TAG.”

 

“Pole kwa familia, Askofu Mkuu Dkt. Barnabas Mtokambali, wana TAG wote, ndugu, jamaa na marafiki. Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina.”

Askofu mwenisongole alikuwa akisumbuliwa na kisukari na shikikizo la damu na msiba upo nyumbani kwake, Mbezi-Mkonde jijini Dar es Salaam.

Mwili wake utaagwa tarehe 29 Desemba 2021, Kanisa la TAG Upanga kuanzia saa 3 asubuhi kisha utasafirishwa kwa maziko yatakayofanyika 30 Desemba 2021, Jimbo la TAG Songwe, Wilaya ya Vwawa mkoani Songwe.

error: Content is protected !!