RAIS wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, amekwenda kuifariji familia ya aliyekuwa Rais wa Taifa hilo, Dk. John Pombe Magufuli, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu
Mama Samia amekwenda kutoa mkono wa pole leo Ijumaa tarehe 19 Machi 2021, mara baada ya kuapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma, kuwa Rais wa sita wa Tanzania.
Amechukua nafasi ya Dk. Magufuli, alifikwa na mauti Jumatano tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena, Makumbusho mkoani Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu ya mfumo wa umeme wa moyo wake.
Mama Samia amemfariji Janeth, mjane wa Dk. Magufuli na binti yake ambapo alipata fursa kuomba dua.

Mama Samia alikuwa ameongozana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Bashiru Ally.
Mara baada ya kutoka kuifariji familia, Mama Samia alikwenda kusaini kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo ya kifo cha Hayati Magufuli (61), katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Leave a comment