Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Samia akutana na mwekezaji Ikulu, atoa maagizo
Habari Mchanganyiko

Rais Samia akutana na mwekezaji Ikulu, atoa maagizo

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa kampuni za Wilmar International ya Singapore, Kuok Khoon Hong. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mazungumzo hayo, yamefanyika leo Ijumaa, tarehe 18 Juni 2021, Ikulu ya Dar es Salaam.

Hong ameahidi kampuni hiyo, ipo tayari kupanua uwekezaji wake katika uzalishaji wa mchele na mafuta kwa kuwa mchele wa Tanzania ni bora na wenye soko kubwa duniani na mahitaji ya mafuta ni makubwa ndani ya nchi.

Amesema kampuni hiyo imefurahishwa na dhamira ya Rais Samia ya kuwavutia zaidi wawekezaji na kwamba tayari imeshawekeza Tanzania kiasi cha Dola za Marekani 150,000,000 katika kiwanda cha kusafisha mafuta ya kula, kutengeneza sabuni na tambi ikiwa ni sehemu ya uwekezaji wa takribani Dola za Marekani Bilioni 1 Barani Afrika.

Mwenyekiti wa kampuni za Wilmar International ya Singapore, Kuok Khoon Hong (katikati)

Kwa sasa kampuni ya Wilmar imekamilisha kujenga kiwanda cha kukoboa mpunga na kufungasha mchele Mkoani Morogoro kitakachokuwa na uwezo wa kukoboa tani 300 za mpunga kwa siku na kutoa ajira kwa watu zaidi ya 1,000.

Akizungumza na mwekezaji huyo, Rais Samia amempongeza Hong kwa uwekezaji wake hapa nchini na amemkaribisha kupanua zaidi uwekezaji huo hususan katika uzalishaji na usindikaji wa mafuta ya alizeti, michikichi na kilimo cha umwagiliaji.

Amemueleza Tanzania ipo tayari kushirikiana na kampuni hiyo katika uwekezaji huo na ameagiza Wizara ya Kilimo na Wizara ya Fedha na Mipango kuandaa andiko la pamoja na kampuni hiyo litakalowezesha ushirikiano huo hususan katika kupata teknolojia, mbegu na mitaji.

Aidha, Rais Samia ametoa wito kwa wawekezaji wengine kuja kuwekeza nchini Tanzania hasa katika sekta ya kilimo kwa kuwa Tanzania ina eneo kubwa linalofaa kwa kilimo na ambalo halitumiki ipasavyo.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda, Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dk. Ramadhan Dau, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Emmanuel Tutuba na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Alphayo Kidata.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!