January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia akumbushia kuku walivyochomwa mipakani, awaweka mtegoni mawaziri

Spread the love

 

Rais Samia Suluhu Hassani amesema amekubaliana na Rais Yoweri Museveni wa Uganda kwamba mawaziri wa kisekta kutoka pande zote mbili wakutane haraka ili kuondoa vikwazo vya kibiashara vilivyopo kati ya Tanzania na Uganda. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Pia amehakikishia Rais Museveni kwamba Serikali ya Tanzania itanunua sukari kutoka nchini humo huku akikosoa kauli ya Waziri aliyesikika kwamba Tanzania haitanunua sukari nje ya nchi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo tarehe 28 Novemba, 2021 katika kongamano la biashara kati Tanzania na Uganda, Rais Samia amesema anataka biashara kati ya Uganda na Tanzania ikue zaidi.

Rais Samia ambaye jana alimpokea Rais Museveni aliyewasili nchini kwa ziara ya siku tatu, alisema Uganda iliiomba Tanzania inunue sukari ya nchi hiyo.

“Rais Museveni amesema hapa aliomba sisi tununue sukari kwake lakini walisikia statement za waziri wetu, kwamba hatutanunua, hatutakubali. That was non-sense, Rais Museveni tutanunua sukari kutoka Uganda,” amesema Rais Samia.

Pamoja na mambo mengine amesisitiza mawaziri wa kisekta kutoka Uganda na Tanzania wakutane haraka kuangalia vikwazo vya kibiashara vilivyopo kati ya pande hizo mbili.

Ametolea mfano sakata la vikwazo vya kibiashara kati ya Kenya na Tanzania namna lililoathiri viumbe hai na kuongeza kuwa sasa biashara kati ya nchi hizo mbili imekua maradufu.

“Tulikuwa tunavutana hapa na Kenya kila kinachokwenda hakipiti, huku hakipiti na kule hakipiti, kule wakizuia na mkuu wa mkoa wetu anasema hakipiti, lakini tulikaa tukaelezana ukweli.

“Tulikuwa tunachomeana kuku mipakani, dhambi tupu… viumbe wa Mungu mnamwagia petroli mnawachoma, haikuwa na maana! Lakini tumeondosha vikwazo sasa biashara imekua mno. Ukiangalia figure za biashara Kenya na Tanzania imekua mno,” amesema Rais Samia.

Pia Rais Samia akizungumzia juu ya mradi wa bomba la mafuta na gesi kati ya Tanzania na Uganda amesema tayari Tanzania imeboresha mazingira ya uwekezaji kwa namna mbalimbali

“Nafarijika kusema jiihada tulizochukua kwa kipindi kifupi cha takribani miezi 8, zimeleta chachu ya kuongezeka uwekezaji na idadi ya ajira zinazotarajiwa kutokana na miradi iliyoandikishwa.

“Tuendelee kukuza uwekezaji katika nyanja mbalimbali ikiwemo viwanda vinavyotumia malighafi za ndani na viwanda vinavyotumia nguvu kazi zaidi ili kuongeza ajira, pamoja na viwanda vinavyozalisha viwanda vingine kama vya mbolea na kemikali.

”Tumefanya marekebisho ya sheria ya kuratibu ajira za wageni, ambapo kwasasa sheria inaruhusu mwekezaji kuingiza wataalam hadi 10 kutoka idadi ya watano iliyokuwa kabla Oktoba 2021.

“Maboresho yamepelekea kupungua kwa muda wa upatikanaji wa vibali vya kazi kwa kuondoa urasimu na sasa hata ndani ya siku moja mwombaji anaweza kupata kibali kupitia mfumo wa E-Permit. Mfumo huu pia unaruhusu upatikanaji kibali cha ukaazi katika kadi moja,” amesema.

Kwa upande wake Rais Museveni amesema tatizo kubwa la nchi za Afrika ni masoko bidhaa zinazotokana na rasilimali asili za nchi husika.

Amsema nchi hizo zimejaaliwa kuwa na rasilimali asili nyingi ambazo hazijatumika ipasavyo.

pAmesema kuwa na rasilimali nyingi sio lazima nchi iwe tajiri kwa sababu hata Uganda wanazo nyingi ila siyo matajiri kwasababu hazijatumiwa ipasavyo.

error: Content is protected !!