RAIS Samia Suluhu Hassan ameonesha kutoridhika na kitendo cha baadhi ya Mawaziri kuajiri maafisa habari binafsi kwaajili ya kuripoti habari zao na si za Serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).
Rais Samia amesema hayo yanafanyika licha ya kila wizara kuwa na kitengo cha mawasilino sambamba na watumishi wa Serikali.
Mkuu huyo wan chi ameyasema hay oleo Alhamisi tarehe 2 Machi 2023 wakati akifungua semina elekezi kwa mawaziri, naibu mawaziri, makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu, inayofanyika jijini Arusha.
“Najua kila wizara ina kitengo cha habari, vitengo hivi vinatumikaje?, vipo tu vimekaa havifanyi kazi lakini bado baadhi yenu Mawaziri mmeajiri maafisa wenu binafsi wa habari wa kutoa taarifa zenu na sio taarifa za Serikali,” amesema Rais Samia na kuongeza;
“Sasa mambo kama haya twende tukarekebishe na nimatumaini yangu kuwa mada kuhusu suala hili litatukumbusha wajibu wetu huo kama viongozi na wasemaji wakuu wa wizara zetu.”
Viongozi hao wakuu wa wizara wanapewa semina hiyo nikiwa ni siku chache tangu Rais Samia kufanya mabadiliko ya baadhi ya wizara kwa kile alichoeleza ni kutoelewana miongoni mwao hivyo kuhitaji kupewa maelekezo ya namna ya utendaji kazi wao.
Leave a comment