May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia aipongeza Tembo Warriors kufuzu kombe la dunia, atoa maagizo

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameitumia salamu za pongeza timu ya taifa ya soka la wenye ulemavu ‘Tembo Warriors’ kwa kufuzu Kombe la Dunia nchini Uturuki 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Ni baada ya leo Jumatano, tarehe 1 Desemba 2021, Tembo Warriors kuishushia kipigo cha 5-0 timu ya Cameroon, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Kufuatia ushindi huo, Tembo wametinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Soka ya Bara la Afrika kwa wenye ulemavu (CANAF 2021) inayoendelea nchini Tanzania.

https://twitter.com/SuluhuSamia/status/1466022390866100229

Timu nne ambazo zinatinga hatua ya nusu fainali ya CANAF 2021, zinafuzu moja kwa moja michuano ya kombe la dunia.

Kufuatia ushindi huo, Rais Samia ametumia ukurasa wake wa Twitter kutoa pongezi hizo kwa Tembo, wizara ya utamaduni, sanaa na michezo pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kufanikisha ushindi huo.

Rais Samia ameandika “naipongeza timu ya Taifa ya Walemavu ya Mpira wa Miguu (Tembo Warriors) kwa kufuzu Kombe la Dunia nchini Uturuki Oktoba, 2022.”

“Nawapongeza viongozi wa wizara na TFF na nawataka mfanye maandalizi mazuri zaidi kuelekea michuano hiyo ili tuwe na timu bora itakayotutangaza vyema.

error: Content is protected !!