RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi watatu akiwemo Mavere Tukai kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …. (endelea).
Tukai anachukua nafasi ya Brig. Jen. Dk. Gabriel Mhidize.
Uteuzi huo umetangazwa usiku wa Alhamisi tarehe 14 Aprili 2022 na Zuhura Yunus, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu akiwa Washington DC nchini Marekani.
Rais Samia yupo Marekani kwa ziara ya kikazi.
Ziara ya rais kikazi wiki mbili? Serious? Yaani anafanya kazi za mawaziri, wakurugenzi na mabalozi?
Raisi wetu yuko makini sana mimi nimtakie majumu endelevu mungu awe upande wako