Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia aiomba benki ya dunia…
Habari za Siasa

Rais Samia aiomba benki ya dunia…

Spread the love

 

SAMIA Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania, ameiomba Benki ya Dunia (WB), kuendelea kushirikiana katika kujenga uchumi utakaogusa makundi yote ya jamii ili kuwafikia watu masikini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Rais Samia ametoa ombi hilo leo Jumatatu, tarehe 19 Aprili 2021, alipokuata na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Mara Warwick, Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma.

Katika mazungumzo hayo, Rais Samia, ameishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kuwa mshirika mzuri wa maendeleo ya Tanzania.

Amemhakikishia, Warwick kuwa, Serikali ya awamu ya sita, itaendeleza na kukuza zaidi ushirikiano wake na benki hiyo katika juhudi zake za kukuza uchumi na kuinua ustawi wa wananchi wa Tanzania.

Rais Samia, ameiomba Benki ya Dunia, kuendelea kushirikiana na Tanzania (Bara na Zanzibar), katika kujenga uchumi utakaoyagusa makundi yote ya jamii hususani kuwafikia watu masikini.

Pia, kuboresha huduma za kijamii hususani elimu na afya, kuimarisha miundombinu, kuwawezesha wanawake kiuchumi ambao wamebeba majukumu makubwa ya familia, na kujenga mifumo ya kidijiti itakayorahisisha utendaji kazi ikiwemo ukusanyaji wa mapato.

Kwa upande wake, Warwick amemshukuru Rais Samia kwa kupata nafasi ya kuzungumza nae na amemhakikishia kuwa Benki ya Dunia ambayo imeanza uhusiano wake na Tanzania tangu miaka 56 iliyopita, itaendelea kushirikiana na Tanzania katika juhudi za kukuza uchumi na ustawi wa jamii huku ikizingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025.

Amesema, benki hiyo itaendelea kujikita kuwasaidia watu masikini na watu waishio katika mazingira hatarishi kwa kuhakikisha, inashiriki kuimarisha miundombinu, masoko, elimu ya msingi, sekondari na vyuo, kuweka mifumo ya kidijiti na kwa Zanzibar kusaidia katika mradi wa nishati ya umeme na uboreshaji wa miji na vijiji.

Warwick amesema, kwa sasa Benki ya Dunia imeidhinisha miradi yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 4.9 (sawa na Sh.11.2 Trilioni), inaelekea kuongeza miradi mingine mitano yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.15 (sawa na Sh.2.6 Trilioni) na mwaka ujao itaongeza zaidi hivyo kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye miradi mingi na muhimu inayofadhiliwa na benki hiyo..

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!