Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari Rais Samia aifagilia TLS “tutakwenda sambamba”
Habari

Rais Samia aifagilia TLS “tutakwenda sambamba”

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali itakwenda sambamba na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), kwa kuwa inajitambua na inaelekea kwenye lengo la kuundwa kwake. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Rais Samia, leo Jumatano, tarehe 22 Februari 2022, akihutubia katika kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini, yaliyofanyika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

“Kwa kweli niipongeze sana TLS kwa kujitambua, sasa TLS inajitambua na inaelekea kule ambako ni lengo la kuundwa kwa TLS. Lakini katikati hapa TLS nadhani mnajua mlichokuwa mnakifanya na kwa maana hiyo Serikali iko pamoja nanyi na tutakwenda sambamba,” amesema Rais Samia.

Wakati huo huo, Rais Samia amemuagiza Waziri wa Katiba na Sheria, George Simbachawene, alifanyie kazi ombi la Rais wa TLS, Prof. Edward Hoseah la uundwaji chama kimoja cha mawakili wa umma na wa sekta binafsi.

“Nimesikiliza pia hotuba ya TLS na nimepokeka maombi yao ya kukatia ardhi Dodoma, lakini pia umeomba tuunganishe kada ya mawakili wa umma walio ndani ya sekta yenu. Waziri yuko hapa mtakwenda kuliangalia muone mnaweza kufanya vizuri zaidi ili liwezekane,” amesema Rais Samia.

“Nimesikiliza pia hotuba ya TLS na nimepoeka maombi yao kwan akuatiw aarhdi dom ambalo jaji feleshi amelimaliza hapahapa,

Pia, Rais Samia amesema analifanyia kazi ombi la Prof. Hoseah la Serikali kutumia mawakili wazawa badala wa kutoka nje ya nchi ili kuokoa gharama.

“Umetuambai Serikali tutumie TLS kabla ya kutumia mawakili kutoka nje na hili naliusianisha na na lile mlilosema kwamba sasa mnajenga vituo maeneo mbalimbali Tanzania, vya kutoa huduma za kisheria,” amesema Rais Samia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!