RAIS Dk.Samia Suluhu Hassan ameibeba tena klabu ya Yanga baada ya kutangaza dau nono la Sh 20 milioni katika mechi za fainali ya Kombe la Shirikisho itakayopigwa tarehe 28 Mei 2023 na marudiano tarehe 3 Juni 2023.
Rais Samia amesema kila bao la ushindi atalipa Sh. 20 milioni lakini pia atatoa ndege ya serikali kuipeleka timu hiyo nchini Algeria kwa ajili ya kumenyana na wapinzani wao USM Alger. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).
Timu mbili hizo zinatarajiwa kukwaana katika mechi mbili za fainali ya Kombe la Shirikisho, mechi inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Yanga na Watanzania kwa ujumla kuishuhudia ikiweka historia ya kutwaa taji hilo linaloratibiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Akizungumza katika tukio la uzinduzi wa Mradi wa Minara ya kurusha matangazo ya Televisheni ardhini (DTT) ya Kampuni ya Azam, Rais Samia alisema uamuzi huo unatokana na matamanio yake ya kuona timu ya Tanzania inafanya vizuri katika michuano hiyo mikubwa barani Afrika.
“Nilianza kwa kutoa Sh. tano milioni kila goli kwa timu ya Simba na Yanga kwenye michuano hii, lakini pia nikatoa Sh. 10 milioni kila goli moja ambapo bahati mbaya Simba wao wameishia njiani na kuwaacha wenzao Yanga.
Uamuzi wa Rais Samia kutoa mamilioni kwa timu za Simba na Yanga umechangia kwa kiasi kikubwa kuzipaisha timu hizo sambamba na kutangaza soka la Tanzania, ambapo Yanga kwa mara ya kwanza ikifanikiwa kufuzu hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho.
Leave a comment