Tuesday , 16 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia ahoji fedha za Plea-Bargaining
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ahoji fedha za Plea-Bargaining

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan, ameitaka Tume ya kuangalia namna ya kuboresha taasisi za haki jinai, ikapitie mchakato kisheria wa makubaliano ya kukiri kosa (Plea Brgaining), uliofanyika kati ya mtuhumiwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashkata nchini (DPP), ili kubaini mahali zilipo fedha zilizokusanywa kupitia zoezi hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Akizungumza wakati anazindua tume hiyo, leo Jumanne, tarehe 31 Januari 2023, Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, Rais Samia amesema kuna kiasi cha fedha kinajulikana kilipo huku kiasi kingine hakionekani mahali kilipo.

Rais Samia amesema kuwa, kuna ufuatiliaji ulifanyika na kubaini kwamba kiasi cha fedha kilibainika kuwekwa katika akaunti nchini China.

“Mkaangalie katika ofisi ya mashtaka na penyewe kukoje, kuna kasoro zipi zimetokea sababu nakumbuka nyuma hapa kidogo Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kulikuwa na ngoma kubwa inachezwa mpaka kukusanya fedha. Zile fedha za Plea Bargaining nyingine zimeonekana na nyingine hazionekani, tuki-trace utaambiwa kuna akaunti China, sijui imepeleka pesa. Tukayatizame,” amesema Rais Samia.

Utaratibu wa Plea Brgaining ulishika kasi katika uongozi uliopita ambapo aliyekuwa DPP Biswalo Mganga, aliongoza zoezi hilo ambalo lilipelekea ofisi yake kukusanya mabilioni ya fedha kutoka kwa watuhumiwa waliokuwa tayari kukiri makosa waliyofanya hasa ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha.

Lakini alipoingia madarakani, Rais Samia aliagiza uchunguzi ufanyike dhidi ya fedha hizo kwa ajili ya kuangalia kama haki ilitendeka, baada ya baadhi ya wahusika kudai kwamba walilazimishwa kutoa fedha hizo kinyume cha sheria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Nape: Wanasiasa, wanahabari, wafanyabiashara mteteeni Samia

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,...

Habari za Siasa

CAG: TAWA imegawa vibali vya uwindaji bila idhini ya waziri

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

Habari za Siasa

TAMISEMI yatenga bil. 17.79 kwa ajili uchaguzi serikali za mitaa

Spread the loveWIZARA Ofisi ya Rais-TAMISEMI, imetenga fedha kiasi cha Sh. 17.79...

Habari za Siasa

CAG abaini madudu katika vyama 10 vya upinzani

Spread the loveUKAGUZI wa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!